RUWASA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WAJA NA MKAKATI WA KUSHUGHULIKIA SUALA LA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

RUWASA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WAJA NA MKAKATI WA KUSHUGHULIKIA SUALA LA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI
Morogoro Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Maji, Afya na Usafi wa Mazingira, umeanza rasmi mchakato wa kuandaa Mkakati wa RUWASA wa Menejimenti ya Tope Kinyesi (Faecal Sludge Management Strategy), unaolenga kuweka mfumo madhubuti, salama na endelevu wa menejimenti ya tope kinyesi katika maeneo ya vijijini. Akifungua Kikao Kazi cha National Task Force kinachofanyika mjini Morogoro, Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Wolta S. Kirita, amesema maandalizi ya Mkakati huo ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za usafi wa mazingira vijijini na kupunguza athari za kiafya na kimazingira zinazoweza kusababishwa na menejimenti isiyo salama ya tope kinyesi. Eng. Kirita amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau katika kuhakikisha Mkakati utakaoandaliwa unazingatia mazingira halisi ya vijijini, unaweka bayana majukumu ya wadau mbalimbali na, muhimu zaidi, unatekelezeka na kuwa endelevu. “Pamoja na jukumu letu kubwa la kuhakikisha w…