RUVUMA YAZINDUA MSINGITEK KUBORESHA STADI ZA KKK KWA TEKNOLOJIA
RUVUMA YAZINDUA MSINGITEK KUBORESHA STADI ZA KKK KWA TEKNOLOJIA
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Adv.Marry Makondo Akizungumza katika uzinduzi wa MsingiTek uliofanyika Mkoani Ruvuma kwa lengo la kuboresha ujifunzaji wa wanafunzi wa shule za msingi Wanafunzi wa Shule ya msingi Humbaro ambapo uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika shule hiyo na katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma Adv.Marry Makondo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed . Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma Mkoa wa Ruvuma umezindua rasmi mradi wa MsingiTek unaotumia teknolojia ya kidijitali kuboresha ujifunzaji wa wanafunzi wa shule za msingi, hususani katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), huku mpango huo ukilenga kufikisha huduma hiyo katika shule 100 za mkoa huo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2026. Uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika shule ya msingi Humbaro na kufanywa na katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Adv. Mary Makondo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Brigedia Jenerali Ahmed Abasi Ahmed. Akizungumza katika hafla hiyo, Makondo amesema MsingiTek ni miongoni …