RC MAKALLA AKAGUA UJENZI WA UPANUZI UWANJA WA NDEGE MANYARA
RC MAKALLA AKAGUA UJENZI WA UPANUZI UWANJA WA NDEGE MANYARA Amtaka mkandarasi kuongeza kasi na kukamilisha kabla ya AFCON 2027 Amshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutoa fedha Bilioni 88 za ujenzi huo …………. Na Mwandishi Maalumu RS Arusha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Lake Manyara wilaya ya Karatu, kutarahisisha usafiri kwa watalii wanaokwenda kwenye hifadhi na mbuga za wanyama pamoja na kupanua wigo wa idadi na ukubwa wa ndege kutua. Mhe. Makalla amesema hayo, alipotembelea na kikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, Agosti 27, 2026 na kubainisha kuwa, mradi huo utawezesha kutua kwa ndege zenye uwezo wa kubeba hadi abiria 40, huku uwepo wa taa na lami ukiongeza usalama na uhakika wa kutua kwa ndege usiku. “Faida za mradi huu ni pamoja na kuongeza idadi ya watalii na abiria, itaongeza pia aina na idadi ya ndege ikiwemo ndege zenye abiria kuanzia 40, zaidi uwepo wa taa utaongeza usalama wa abiria kutua kwa uhakika kwani taa na lami zitasaidia usalama.” Amesema C…