RAIS SAMIA : TUITUNZE AMANI KWANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO

RAIS SAMIA : TUITUNZE AMANI KWANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa wananchi kulinda amani kama msingi mkuu wa maendeleo na kuenzi dhana ya mapinduzi ili iwe chachu ya kuleta mabadiliko bora ya kiuchumi na kijamii.  Alisema wananchi wanapaswa kuendelea kuitunza amani na kuenzi dhana ya mapinduzi kwa kuhakikisha inakuwa chachu ya maendeleo. “Tunaposema Mapinduzi daima, Mapinduzi ya juzi ni ya maendeleo. Tunapindua yaliyokuwepo ambayo tulikuwa nyuma, tunaleta maendeleo bora zaidi. Hiyo ndiyo maana ya Mapinduzi,” alisema Rais Samia. Alihimiza wananchi wawe walinzi wa miundombinu, ikiwemo ya mradi wa maji kwa kuwa zimetumika fedha nyingi na utaalamu. “Miradi hii ni uhai wetu, ni fursa zetu, ni uchumi wetu na ustawi wa maisha yetu… Ni wajibu wetu na ni lazima ndugu zangu tuitunze miradi hii kama tunavyotunza macho yetu,” alisema Rais Samia. Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji wa Kizimkazi wakati wa Tamasha la Kizimkazi, Rais Samia alisema amani imewezesha kupata maendeleo, hivyo wananchi wailin…