Posts

RAIS SAMIA: AFRIKA IHARAKISHE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MIUNDOMBINU ILI KUCHOCHEA UCHUMI NA AJIRA

RAIS SAMIA: AFRIKA IHARAKISHE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MIUNDOMBINU ILI KUCHOCHEA UCHUMI NA AJIRA
Na Janeth Raphael -MichuziTv  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa viongozi wa nchi za Afrika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya miundombinu, akisisitiza kuwa maendeleo ya Bara hilo hayatapimwa kwa mipango na sera pekee, bali kwa matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi. Rais Samia ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Jukwaa la Miundombinu Afrika pamoja na Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Africa50, ambapo alieleza kuwa uwekezaji katika miundombinu ni nguzo muhimu ya kukuza uchumi, kuongeza ushindani wa Afrika, kuvutia wawekezaji na kuimarisha biashara ndani ya bara. Amesema wananchi wanahitaji kuona matokeo kupitia ujenzi wa barabara bora, reli za kisasa, bandari zenye ufanisi, nishati ya uhakika, maendeleo ya teknolojia pamoja na kuongezeka kwa fursa za ajira. Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na Tanzania, Rais Samia alisema Serikali inaendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi wa vi…