Posts

PPAA YAWANOA WAKANDARASI MAZINGIRA YA HAKI MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA

PPAA YAWANOA WAKANDARASI MAZINGIRA YA HAKI MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA
Na Mwandishi Wetu, Dar Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewajengea uwezo makandarasi kuhusu mazingira ya haki katika mchakato wa zabuni za umma, ili waweze kudai haki zao pindi wanapoona hawakutendewa haki kwenye michakato ya zabuni za umma walizoshiriki. Wasilisho la PPAA limewasilishwa na Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi ambaye alimwakilisha Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando katika Mkutano wa Mashauriano na Wadau wa Sekta ya Ujenzi kwa Mwaka 2026 ulioandaliwa na Bodi ya Wakandarasi (CRB) tarehe 13 – 14, Agosti, 2026 Jijini Dar es Salaam.  Bi. Sayi amesema kuwa, ununuzi wa umma ni zaidi ya utaratibu wa kununua kazi za ujenzi, bidhaa au huduma; ni chombo cha sera ya maendeleo kinachochochea ukuaji wa uchumi, ajira, kuwezesha makandarasi wazawa kushiriki katika miradi ya Serikali na kuhakikisha matumizi bora ya fedha za umma.  “Mazingira ya haki katika mchakato wa zabuni za umma ni mfumo unaohakikisha washiriki wote wanatendewa kwa usawa, wanashinda…