OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWANOA WABUNGE KUHUSU BIASHARA YA KABONI

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWANOA WABUNGE KUHUSU BIASHARA YA KABONI
Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) imetoa mafunzo kwa Wabunge kuhusu Biashara ya Kaboni, Mafanikio, Changamoto na Hatua za Utatuzi wake. Mafunzo hayo yaliyofanyika leo Agosti 13, 2026 jijini Dodoma yametolewa kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Maji Mazingira. Akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alisema ili miradi ya kaboni iendelee kufanyika kwa ufanisi ni muhimu mifumo ikasomana. Dkt. Ndumbaro ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini alisema Ofisi ya Makamu ni muhimu kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii yenye dhamana ya misitu pamoja na Wizara ya Nishati ambayo ina jukumu la kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za nishati. Aliongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wabunge kwakuwa wao ndio wawakilishi wa wananchi katika maeneo yao hivyo itakuwa rahisi kufikisha ujumbe kwa urahisi. Kwa upande wake Makamu Mw…