NM-AIST KINARA WA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI 2026

NM-AIST KINARA WA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI 2026
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) imeibuka kinara miongoni mwa Taasisi za Elimu katika Maonesho ya 33 ya Kilimo, Mifugo na Sherehe za Nanenane Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika Viwanja vya Themi Njiro, Arusha. Akizungumzia ushindi huo, Prof. Maulilio Kipanyula, Makamu Mkuu wa NM-AIST, amesema bidhaa bora zinahitaji utafiti na NM-AIST kama Taasisi inayotanguliza ubunifu, imeendelea kubadilisha matokeo ya tafiti kuwa teknolojia zinazotoa suluhisho kwa changamoto za wakulima na wafugaji. Amesema teknolojia mbalimbali zinazooneshwa na Taasisi, ikiwemo Mfumo wa Ng’ombe Smart, zinalenga kuongeza tija katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kwa kuwezesha ufuatiliaji wa uzalishaji wa maziwa na taarifa muhimu za mifugo. Aidha, Prof Kipanyula amesema mwaka huu NM-AIST imekuja na teknolojia zinazolenga kuongeza thamani ya mazao, yakiwemo tumbaku, mazao ya chakula pamoja na vyakula vya mifugo kama kuku na ng’ombe. Prof. Kipanyula amesisitiza kuwa NM-AIST inaende…