NI DHAMBI KUBWA KWA MWANAUME WA KIHADZABE KUTAHIRIWA
NI DHAMBI KUBWA KWA MWANAUME WA KIHADZABE KUTAHIRIWA Wahadzabe ni kabila linalopatikana mkabala na ziwa Eyasi pembezoni mwa hifadhi ya Ngorongoro na habari za maisha yao zimehifadhiwa katika makumbusho ya Urithi Jiopaki liyopo Karatu Mkoani Arusha. Pamoja na mabadiliko ya ulimwengu na elimu kutolewa lakini kabila hili bado haliamini katika tohara kwa kijana wa kiume, kwao hiyo ni mwiko wakiamini binadamu anastahili kuwa kama alivyozaliwa. Sababu kubwa ya kutokutahiriwa ni kuwa ukitahiriwa unapunguza nyama ya binadamu na kuizika wakati binadamu huyo akiwa hai, imani ni kwamba huwezi kata sehemu yoyote ya mwili wa binadamu aliye hai Vilevile kabila hili linaamini kwamba mwanaume akitahiriwa hupunguza ukubwa na utaalam wa mambo na kufanya mwili wako kuwa na mapungufu hata wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Katika kuhakikisha kwamba mwanaume anakuwa na nguvu za kutosha wakati wa kushiriki tendo la ndoa hulazimika kula mizizi inayopatikana porini , matunda, asali ikiwa fresh na nyama pori ambayo inachomwa au kuchemshwa supu. Kutokana na kutokutah…