NGORONGORO SCHOLARSHIP FUND, TABASABU JIPYA WANAFUNZI KUTOKA HIFADHI YA NGORONGORO.

NGORONGORO SCHOLARSHIP FUND, TABASABU JIPYA WANAFUNZI KUTOKA HIFADHI YA NGORONGORO.
Na Mwandishi Wetu, DSM. Serikali kupitia Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya huu (HESLB) imeanzisha mfuko wa Ngorongoro Scholarship Fund kwa lengo la kuwezesha wanafunzi wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kupata fursa ya masomo ya elimu ya juu kupitia ufadhili Ngorongoro Fund. Akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam kwa niaba ya kamishna wa Uhifadhi, Kamishna msaidizi mwandamizi wa uhifadhi anayesimamia idara ya Maendeleo ya Jamii Gloria Bideberi ameeleza kuwa Program hiyo inalenga kuboresha maisha ya jamii zinazoishi ndani ya hifadhi, ambapo kwa kushirikiana na bodi ya mikopo ya elimu ya juu watahakikisha kila mtoto anayeishi ndani ya hifadhi hiyo anayekidhi vigezo anapata nafasi ya kupata ufadhili wa elimu ya juu. “Kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ufadhili huu utasaidia kuondoa malalamiko ya upendeleo, taratibu zote za ufadhili wa vijana wetu zitakuwa wazi kwa ku…