NGORONGORO NA SIMBA DAY NI BAO LA KISIGINO
Waswahili husema Chanda chema huvikwa pete msemo ambao umedhihirika siku ya mnyama “Simba Day “ baada ya klabu hiyo kumtunuku tuzo Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru kutokana na mchango wake mkubwa wa kuunganisha utalii na michezo. Kamishna Badru amekabidhiwa tuzo hiyo kutokana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kukubali na kushiriki kikamilifu maadhimisho ya wiki ya simba ambapo mamlaka ilitumia fursa hiyo kutangaza shughuli zake za uhifadhi na utalii na kukaribisha wadau mbalimbali kurudi nyumbani Ngorongoro Dhamira ya Kamishna Badru ni kuhakikisha kuwa utalii wa Ngorongoro na michezo unafungamanishwa sambamba ambapo tarehe 13 Julai,2026 mamlaka hiyo na klabu ya Simba ziliafikiana kushirikiana katika tukio hilo lenye mamilioni ya watazamaji ndani na nje ya nchi ambalo uzinduzi wake ulifanyika tarehe 1 agosti, 2026 ndani ya Kasoko ya Ngorongoro. “Chapa hizi mbili kubwa kimataifa zinaafikiana katika jambo hili kwa kuwa tunataka kutangaza utalii wa…