NGORONGORO KIVUTIO CHA UTALII KILICHOTEMBELEWA ZAIDI MWAKA 2025.

NGORONGORO KIVUTIO CHA UTALII KILICHOTEMBELEWA ZAIDI MWAKA 2025.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro limetajwa kuwa ndio kivutio namba moja kilichotembelewa zaidi na watalii kwa mwaka 2025 ambapo watalii 859,933 walitembelea hifadhi hiyo ambayo ni kivutio namba moja cha utalii barani afrika. Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyofanya  utafiti wa wageni wa kimataifa wakati wa kuondoka  mwaka 2025 (The 2025 International visitors Exit Survey report) inaOnyesha kuwa eneo la hifadhi ya Ngorongoro limetembelewa na asilimia 14.2 ya wageni waliowasili chini kwa mwaka huo na kuwa kinara katika maeneo yote ya utalii nchini. Ongezeko la idadi ya wageni katika hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine ya nchi inatokana na jitihada za serikali na wadau wa utalii kuendelea kuitangaza Tanzania katika majukwaa na maonesho ya kimataifa huku Ngorongoro ikiboresha huduma za wageni na kuimarisha miundombinu ya utalii kwenye vivutio vilivyopo ndani ya hifadhi ili kuongeza mtawanyiko wa wageni kwenye vivutio hivyo. Eneo la hifadhi ya Ngorongoro lina vivuti…