NDOTO IMETIMIA NA MPANGO WA KUWA NA UMEME WA UHAKIKA UMEWEZEKANA - RAIS SAMIA

NDOTO IMETIMIA NA MPANGO WA KUWA NA UMEME WA UHAKIKA UMEWEZEKANA - RAIS SAMIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kukamilika kwa Mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere ni utekelezaji wa ndoto ya muda mrefu ya Tanzania ya kuwa na umeme wa uhakika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Rais Samia amesema Serikali ilitekeleza mradi huo kwa uzito unaostahili kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa maendeleo ya Taifa, akieleza kuwa hakukuwa na namna ya kuuacha mradi huo kutokana na mchango wake unaotarajiwa katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini. Akizungumza leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akizindua rasmi mradi huo Mkoani Pwani, Rais Samia amesema ni jambo la furaha kushuhudia kukamilika kwa mradi ambao kwa miaka mingi umekuwa sehemu ya mipango na jitihada za Serikali za kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika. Rais Samia amekumbusha kuwa Desemba 22, 2022 alifika kushuhudia hatua ya kufungwa kwa njia ya kuchepusha maji ya Mto Rufiji na kuanza kujazwa kwa maji katika bwawa hilo, akis…