NDEJEMBI: JNHPP YAONGEZA NGUVU YA TANZANIA KUUZA UMEME NJE
NDEJEMBI: JNHPP YAONGEZA NGUVU YA TANZANIA KUUZA UMEME NJE Na Fullshangwe, Rufiji RUFJI, PWANI: Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kukamilika na kuzinduliwa kwa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) ni matokeo ya juhudi mahususi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuongeza uwezo wa Taifa wa kuzalisha umeme. Akizungumza mbele ya Rais Samia katika hafla ya uzinduzi wa JNHPP wilayani Rufiji, mkoani Pwani, leo Agosti 22, 2026, Ndejembi amesema kituo hicho kina mitambo tisa, ambapo kila mtambo una uwezo wa kuzalisha megawati 235, hivyo kuwa na uwezo wa jumla wa kuzalisha megawati 2,115. Amesema uzalishaji huo umeongeza uwezo wa Tanzania kukidhi mahitaji ya umeme yanayotokana na shughuli za kiuchumi na uwekezaji, huku ikiifanya nchi kuwa daraja muhimu la kuunganisha masoko ya nishati ya umeme barani Afrika kupitia East African Power Pool na Southern African Power Pool. Ndejembi amesema uwezo wa Taifa wa kuzalisha umeme umefikia megawati 4,646 dhidi ya mah…