MWENGE WATEMBELEA HOTELI YA KER BUKOMBE KUHAMASISHA NISHAFI SALAMA YA KUPIKIA

MWENGE WATEMBELEA HOTELI YA KER BUKOMBE KUHAMASISHA NISHAFI SALAMA YA KUPIKIA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndugu Wazo Michael Mwang’onda, leo tarehe 28 Agosti 2026 ametembelea na kuzungumza na wafanyabiashara katika Hoteli ya KER iliyopo Mtaa wa Butambala, Kata ya Igulwa Wilaya ya Bukombe. Ziara hiyo ni sehemu ya Programu ya Nishati Safi na Salama ya Kupikia inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Lengo ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi katika hoteli na migahawa. Akizungumza na wamiliki na wafanyakazi wa Hoteli ya KER, Mwang’onda amesema Serikali ina dhamira ya kuwawezesha wafanyabiashara wa vyakula kutumia nishati safi ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuboresha mazingira ya kazi. Amesema matumizi ya nishati safi kama gesi ni ya ufanisi zaidi, yanaokoa muda na yana afya kuliko kutumia kuni na mkaa. Hii inawasaidia mama lishe na baba lishe kuongeza kipato chao kwa sababu gharama zinapungua na huduma inakuwa ya haraka. Mwang’onda pia amesisitiza umuhimu wa kulinda mazingira. Amesema …