MUHAS, NIMR YAZINDUA UTAFITI WA PROBIOTICS KUBORESHA CHANJO YA ROTAVIRUS NA KUPUNGUZA KUHARA KWA WATOTO
MUHAS, NIMR YAZINDUA UTAFITI WA PROBIOTICS KUBORESHA CHANJO YA ROTAVIRUS NA KUPUNGUZA KUHARA KWA WATOTO Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Sekta ya Afya, Profesa Tumaini Nagu akizungumza na leo, Agosti 18, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduziPRORota Clinical Trial, utafiti wa kitabibu unaolenga kutathmini iwapo matumizi ya probiotics yanaweza kuongeza ufanisi wa chanjo ya rotavirusi. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa MUHAS, Profesa Bruno Sunguya akizungumza na leo, Agosti 18, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi PRORota Clinical Trial, utafiti wa kitabibu unaolenga kutathmini iwapo matumizi ya probiotics yanaweza kuongeza ufanisi wa chanjo ya rotavirusi. ……….. NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) pamoja na taasisi washirika kutoka nje ya nchi, kimezindua PRORota Clinical Trial, utafiti wa kitabibu unaolenga kutathmini iwapo matumizi ya probiotics yanaweza kuongeza ufanisi wa chanjo ya r…