MTAALAM SEKTA YA MAFUTA DK.SAJAD RAI AMPONGEZA MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI
MTAALAM SEKTA YA MAFUTA DK.SAJAD RAI AMPONGEZA MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI
Na Mwandishi Wetu MTAALAM katika Sekta ya Mafuta nchini Dkt Sajad Habib Rai amempongeza Makamu wa Rais Ndejembi kwa kuapishwa kwake kushika nafasi hiyo huku akisisitiza hana shaka na uwezo na uadilifu wake katika kulitumikia Taifa la Tanzania akimsaidia Rais Samia Suluhu Hassan Akizungumza jijini Dar es Salaam siku moja baada ya uapisho wa Makamu Rais huyo Ikulu ya Cha Chamwino, Dodoma, Dkt Sajad amesema ana imani kubwa na Kiongozi huyo huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa Ndejembi. Dkt Sajad ambaye ni Meneja Mkazi wa Mansoor Industries nchini, amesema hana shaka na uwezo wa Ndejembi katika uongozi akisisitiza kwa sifa na uwezo alionao ni msaada tosha katika usaidizi kwa Dkt Samia Suluhu Hassan. " Kwa kipindi kifupi alichohudumu katika Wizara ya Nishati kwa nafasi ya Uwaziri , Mheshimiwa Ndejembi amekuwa mtu muhimu aliyesimama kikamilifu katika kuahughulikia masuala mbalimbali, hii ni sifa ambayo siyo kila Kiongozi anayo" amesema Dkt Sajad Amesema hatua ya R…