MKUTANO MKUU WA TOA WALENGA UTEKELEZAJI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
MKUTANO MKUU WA TOA WALENGA UTEKELEZAJI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 Na: OWM – TAMISEMI, Dodoma Mkutano Mkuu wa 16 wa Mwaka wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unatarajiwa kujadili mchango wa ugatuzi wa madaraka katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku ukilenga kuweka mikakati itakayowezesha wananchi kunufaika zaidi na usimamizi wa maendeleo katika maeneo yao. Mkutano huo utafanyika Agosti 19–21, 2026 katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma, Mji wa Serikali Mtumba, ukiwa na Kaulimbiu isemayo: “Ugatuzi wa Madaraka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni nguzo madhubuti ya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.” Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa TOA, Bw. Albert Gabriel Msovela, ambaye amesema Mgeni Rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye atauzindua rasmi Agosti 19, 2026. Bw. Msovela amesema mkutano huo unaendana na maelekezo ya Serikali yanayochagizwa na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wananufaika n…