MKURUGENZI MTENDAJI WA STANBIC BANK TANZANIA KUZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA INFRA FOR AFFRICA FORUM 2026
DAR ES SALAAM, Tanzania – Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic Bank Tanzania, Manzi Rwegasira, atajumuika na viongozi wa kimataifa, mawaziri, watunga sera, wawekezaji, taasisi za fedha za maendeleo pamoja na viongozi wa biashara katika Mkutano wa Infra for Africa Forum 2026, unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 5 hadi 6 Agosti 2026. Mkutano huo, ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Africa50, utawakutanisha wadau muhimu kujadili mbinu bunifu za kuharakisha maendeleo na uwekezaji katika miundombinu barani Afrika, huku Mgeni Rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tarehe 5 Agosti, Rwegasira atashiriki katika mjadala wa ngazi ya juu wenye mada “Reinvesting for Expansion: Asset Recycling as a Multiplier”, akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Nishati na Miundombinu Duniani wa Standard Bank Group, Dele Kuti, na viongozi wengine waandamizi. Katika mjadala huo atazungumzia ugharamiaji wa miundombinu, uhama…