MKURANGA WATAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA

MKURANGA WATAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nassir Ali, amewataka wananchi wa Mkuranga kuhakikisha wanalinda miundombinu ya gesi asilia iliyojengwa katika maeneo yao ili iweze kudumu na kuwanufaisha wananchi pamoja na taifa kwa ujumla. Amesema ulinzi wa miundombinu hiyo ni jukumu la pamoja, huku akisisitiza wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi. Akizungumza katika bonanza la michezo na upimaji wa afya bure lililoandaliwa na TPDC Kisemvule , Mkuranga, Khadija amesema mradi wa usambazaji wa gesi asilia tayari umewezesha zaidi ya nyumba 500 kuunganishwa na huduma hiyo. Amesema bonanza hilo pia linalenga kuwakutanisha na kuwaunganisha wananchi wa Kisambule na Mkuranga kwa ujumla, sambamba na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi na ulinzi wa miundombinu. Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amesema Mkuranga inajivunia kuwa miongoni mwa maeneo yanayonufaika na uwekezaji mkubwa katika nishati sa…