MEYA NGWADA AITAKA IRINGA KUTUMIA UTALII KUZALISHA AJIRA KWA VIJANA

MEYA NGWADA AITAKA IRINGA KUTUMIA UTALII KUZALISHA AJIRA KWA VIJANA
NA DENIS MLOWE IRINGA  MEYA wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada, amesema utalii ni biashara yenye uwezo mkubwa wa kuchochea uchumi na kuunda ajira kwa vijana, akiwataka wananchi kutumia fursa zilizopo katika vivutio vya utalii vya mkoa huo. Ngwada aliyasema hayo wakati akiwaaga wananchi zaidi ya 70 wanaoshiriki ziara ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa, ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ziara iliyoandaliwa na taasisi ya Iringa Safari Hub. Amesema Manispaa ya Iringa imebahatika kuwa sehemu muhimu ya utalii katika Nyanda za Juu Kusini, hivyo wananchi, hususan vijana, wanapaswa kutumia fursa hiyo kujifunza na kujiandaa kushiriki katika shughuli za utalii. “Utalii ni biashara wenzetu wa maeneo ya Arusha na maeneo mengine wanajenga, wanaishi, wanatibu wazazi wao na wanajitibu wao kupitia utalii na Serikali yetu inafanya jitihada kubwa kuhakikisha inakuza utalii katika maeneo ya kusini,” alisema Ngwada. Alisema Iringa imekuwa kitovu cha utalii katika Nyanda za Juu Kusini,…