MEYA IRINGA APINGA TAARIFA YA KUONGEZA ADA SHULE ZA KIINGEREZA ZA MAPINDUZI,CHIFU MKWAWA NA GANGILONGA
MEYA IRINGA APINGA TAARIFA YA KUONGEZA ADA SHULE ZA KIINGEREZA ZA MAPINDUZI,CHIFU MKWAWA NA GANGILONGA NA DENIS MLOWE IRINGA MEYA wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada, amefuta taarifa iliyokuwa imeeleza kuwa Halmashauri imekubaliana kuongeza ada katika shule za mchepuo wa Kiingereza, ikiwemo Shule ya Msingi Mapinduzi, kutoka Shilingi 300,000 hadi Shilingi 500,000 kwa mwaka. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Meya Ngwada alisema suala la kuongeza ada halijapitishwa na kwamba kumbukumbu zilizowasilishwa zilikuwa na taarifa isiyoendana na uamuzi wa kikao. Alisema awali wataalamu walipewa jukumu la kufanya upembuzi na kuwasilisha mapendekezo kuhusu uwezekano wa kubadili ada, na kwamba suala hilo linapaswa kurejea katika vikao halali vya kisheria kabla ya uamuzi wowote kufanyika. “Hatujapandisha ada kwenye shule zetu za Mapinduzi, Gangilonga na Chifu Mkwawa. zitabaki kuwa zile zile hatujabadilisha ada,” alisema Meya Ngwada. Meya Ngwada aliwataka wazazi na wananchi kutokuwa na hofu, akisisitiza kuwa kwa sasa hakuna ongezeko la ada lililoidhinis…