MBUNGE AZZA AGUSA MAISHA YA WANANCHI NDUGUTI KWA VITENDO

MBUNGE AZZA AGUSA MAISHA YA WANANCHI NDUGUTI KWA VITENDO
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akisalimia na wa wananchi wa Kijiji cha Nduguti Kata ya Nyida wilayani Shinyanga Na Marco Maduhu, SHINYANGA Wananchi wa Kijiji cha Nduguti Kata ya Nyida wilayani Shinyanga, wameelezea furaha yao kwa Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, kwa kuguswa na maisha ya wananchi wake na kuwatatulia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili kwa vitendo, ikiwamo kuwapaulia Zahanati ya kijiji hicho kwa fedha zake za mfukoni. TAZAMA VIDEO 👇👇 Wamebainisha hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Azza wa kusikiliza kero zao akiwa pia ameambatana na wataalamu wa serikali kujibu kero hizo. Mmoja wa wanachi hao Ashura Manyama, amesema wanamshukuru Mbunge huyo kwa kuwapaulia Zahanati ya kijiji hicho, ambalo boma lake limekaa kwa muda mrefu, na kusababisha kukosa huduma za matibabu karibu na maeneo yao. “tunatoa shukrani kwa Mbunge wetu kwa kutupaulia Zahanati yetu ya kijiji cha Nduguti, tangu tumeanza kupata wabunge huyu diyo Mbunge wa kwanza kututend…