KWA MARA YA KWANZA JKCI YAFANYA UPASUAJI WA MYO KWA MTOTO WA SIKU MBILI

KWA MARA YA KWANZA JKCI YAFANYA UPASUAJI WA MYO KWA MTOTO WA SIKU MBILI
Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imefanikiwa kumfanyia upasuaji wa moyo mtoto wa siku mbili aliyezaliwa akiwa na tatizo la kubana kwa mshipa wa damu unaopeleka damu kwenye mapafu (Severe pulmonary valve stenosis). Upasuaji huo wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Percutaneous balloon pulmonary valvuloplasty- PBV) umefanyika akatika kambi maalumu ya siku sita iliyokuwa ikifanywa na watalaamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa shirika la Muntada Aid lililopo nchini Uingereza. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya alisema ushirikiano huo wa kimatibabu umeleta matokeo makubwa ikiwemo kufanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto wa siku mbili. “Hii ni mara yetu ya kwanza kumfanyia mtoto wa umri huu, mafanikio haya ni matokeo ya msaada wa vifaa tiba uliofanywa na shirika hili pamoja na serikali yetu ya Tanzania kwa kuweka mazingira…