KUTANA NA 'ORIGIN' POMBE YA MITI SHAMBA!

KUTANA NA 'ORIGIN' POMBE YA MITI SHAMBA!
Dar es Salaam | 31 Julai 2026 Kwa wiki kadhaa, swali moja limekuwa likiulizwa kila sehemu—mitandaoni, kwenye WhatsApp, hata pale unapokutana na marafiki kwenye baa. Watu wamekuwa wakiuliza: "Kwa nini mitishamba inazungumzwa sana hivi karibuni?" Wengine walidhani ni dawa mpya. Wengine walisema labda ni filamu. Wengi hawakujua. Sasa jibu limefika. Serengeti Breweries Limited imezindua ORIJIN . Ni pombe, lakini pombe inayotokana na mitishamba ya Kiafrika—herbs, roots na fruits ambazo Watanzania wamekua nazo, ambazo bibi zetu walizungumza nazo. Kabla ORIJIN haijafahamika, kampeni ya ORIJINO MITISHAMBA ilikuwa imeshaanzisha mazungumzo. Watu walishiriki uzoefu wao. Wengine wakasimulia hadithi za bibi zao. Wengine wakielezea jinsi mitishamba ilivyowasaidia. Wengine wakibishana kuhusu nini ina nguvu kuliko nini. Lakini hakuna aliyefahamu kwamba yote yalikuwa yakipelekea kitu. Siri ilikuwa inajengwa. Na leo, imefichuliwa. ORIJIN inaleta ladha ya uchungu na utamu, kama mitishamba mingi unayoiju…