KUNDEMBA FC MABINGWA PBZ YAMLE YAMLE CUP, MASAUNI AWAPA 10M

KUNDEMBA FC MABINGWA PBZ YAMLE YAMLE CUP, MASAUNI AWAPA 10M
Na; Mwandishi Wetu  Unguja TIMU ya Kundemba FC imetawazwa mabingwa wapya wa Mashindano ya PBZ Yamle Yamye kwa kuichapa bao 1-0 timu ya Ubinadam Kazi FC lililofungwa na Abdallah IddI Pina katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mashindano hayo yalishirikisha timu 36 kutoka Unguja timu 24 na Pemba timu 12 yakiwa katika msimu wa nane, hivyo kuifanya Kundemba FC kuzawadiwa kitita cha Shilingi 20M huku mshindi wa pili akikabidhiwa kiasi cha Shilingi 10M. Pamoja na Kundemba FC kuzawadiwa kiasi hicho cha fedha kama bingwa lakini mlezi wa timu hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Mhe. Hamad Yussuf Masauni inapotokea timu hiyo aliwapongeza kwa kuwapa kiasi cha shilingi 10M. Mhe. Masauni ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) amesema ataendelea kuisapoti timu hiyo ili kuona vijana wananufaika na vipaji vyao kupitia mchezo wa soka. “Soka ni moja ya ajira ambayo watu wanalipwa fedha nyingi, ndio maana serikali kwa kutambua hilo imeweka maz…