KLINIKI YA WATUMISHI IRINGA YAIBUA MATUMAINI KWA WATUMISHI NA WASTAAFU

KLINIKI YA WATUMISHI IRINGA YAIBUA MATUMAINI KWA WATUMISHI NA WASTAAFU
NA DENIS MLOWE IRINGA MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amezindua Kliniki ya Watumishi wa Umma inayolenga kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili watumishi na wastaafu katika Mkoa wa Iringa, akisisitiza kuwa utatuzi wa changamoto za watumishi ni msingi wa kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kliniki hiyo uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma kupitia maboresho ya mishahara, upandishaji wa madaraja, ajira mpya na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa rasilimali watu. Alisema pamoja na hatua hizo, bado zipo changamoto zinazowakabili baadhi ya watumishi na wastaafu, ikiwemo malimbikizo ya mishahara, madai ya likizo, uhamisho, matibabu, kupandishwa madaraja, mafao ya wastaafu pamoja na fidia kwa watumishi wanaoumia kazini. “Lengo la kliniki hii siyo kutafuta makosa ya watu, bali kutafuta s…