KAMPENI YA TUMAINI KUWAFIKIA WAJAWAZITO, YAS YAANZA NA HOSPITALI YA UBUNGO
KAMPENI YA TUMAINI KUWAFIKIA WAJAWAZITO, YAS YAANZA NA HOSPITALI YA UBUNGO Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Yas Tanzania, Caroline Kavishe (kushoto), akikabidhi vifaa tiba kwa Mkuu wa Kitengo cha Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Dkt. Olivia Donald Shirima, ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Tumaini inayoendeshwa na wafanyakazi wa Yas kwa lengo la kusaidia wajawazito na akina mama. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Dkt. Chrispin Kayola. ………… Dar es Salaam, 28 Agosti 2026 – Wajawazito wanaopata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, watanufaika na vifaa vya kujifungulia pamoja na vifaa tiba vilivyotolewa na wafanyakazi wa Yas Tanzania katika jitihada za kumshika mkono akina mama wajawazito. Msaada huo umetolewa kupitia Kampeni ya Tumaini, ambao ni mpango ulioanzishwa na wafanyakazi wa Yas, umeanza na hospitali hiyo huku ukitarajiwa kuendelea katika maeneo mengine mbalimbali nchini. Kupitia kampeni hiyo, Yas imekabidh…