KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA RUZUKU KWA TBA

KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA RUZUKU KWA TBA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiomba Serikali kuongeza ruzuku kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ili kuwezesha kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma nchini. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya nyumba za watumishi inayotekelezwa na TBA katika maeneo ya Kisasa na Nzuguni jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kutathmini utekelezaji wa miradi ya miundombinu nchini. Kakoso amesema Kamati imejiridhisha na juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na TBA katika kukabiliana na changamoto ya makazi kwa watumishi wa umma, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya ujenzi kutokana na mahitaji makubwa ya nyumba nchini. Amesema eneo la Nzuguni lenye takribani ekari 630 lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ni hatua muhimu katika kuendeleza mji mpya wa Serikali, kwa kuwa uwepo wa nyumba hizo utawasaidia watumishi, wakiwemo walio katika ngazi za chini, kupata makazi yaliyo karibu …