KAIRUKI: SERIKALI KUYAFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA HAKI ZA ARDHI ZA WANAWAKE

KAIRUKI: SERIKALI KUYAFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA HAKI ZA ARDHI ZA WANAWAKE
Na Meleka Kulwa — Fullshangwe Blog, Dodoma Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Kairuki, amesema Serikali itayafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa katika Kongamano la Haki za Ardhi za Wanawake, huku akiahidi kuyawasilisha katika majukwaa ya kitaifa na kimataifa ili kuimarisha ushiriki wa wanawake katika masuala ya ardhi, mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Ameyasema hayo Agosti 13, 2026, jijini Dodoma wakati akifunga kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili, Agosti 12 hadi 13, likiwakutanisha viongozi wa Serikali, wataalamu wa ardhi, wadau wa maendeleo na viongozi wa wanawake. Huku akibainisha Kuwa kongamano hilo limewezesha wadau kutengeneza mapendekezo yanayolenga kuimarisha utekelezaji wa sheria za ardhi, kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi, kuimarisha mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijini na kuongeza uwekezaji katika miradi ya wanawake na vijana. Aidha, amesema mapendekezo hayo yamegusa umuhimu wa kuhakikisha fedha za kukabiliana …