IAA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA ILI KUENDELEA KUZALISHA WATAALAM MAHIRI
IAA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA ILI KUENDELEA KUZALISHA WATAALAM MAHIRI
Na Mwandishi Wetu MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka amesema IAA itaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira ya kujifunzia ili kandaa watalaam mahiri na kuendana na mahitaji ya programu za kisasa hususani programu zinazohusisha matumizi makubwa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Prof. Sedoyeka amesema hayo Agosti 24, 2026 katika hafla ya uzinduzi wa utoaji wa programu za Shahada ya Uhasibu na Teknolojia ya Habari (Bachelor Degree in Accountancy with IT) na Shahada ya Sayansi ya Kompyuta (Bachelor Degree in Computer Science) katika Kampasi ya Babati iliyofanyika Waangw’aray Mjini Babati. “Tunaishukuru Serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) imetoa jumla ya shilingi bilioni 13.7 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala, mkataba na maabara ya TEHAMA katika Kampasi ya Babati. Sisi pia tumewekeza katika teknolojia na mkakati wetu ni madarasa yetu yote yawe ‘smart classes’ madarasa janja” amesema. Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa d…