HISABATI YAUNGANISHA DUNIA ARUSHA, WATAALAMU WAJADILI NAFASI YAKE KATIKA MAENDELEO
HISABATI YAUNGANISHA DUNIA ARUSHA, WATAALAMU WAJADILI NAFASI YAKE KATIKA MAENDELEO Mratibu Msaidizi wa Idara ya Hesabu na Mhadhiri wa UDSM, Dkt. Sylivesta Rugeiyhamu akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha . Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. William Anangisye akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha. Happy Lazaro,Arusha ARUSHA. Wataalamu wa hisabati kutoka Afrika na nchi mbalimbali duniani wamekutana jijini Arusha katika mkutano wa pili unaolenga kuimarisha taaluma hiyo, utafiti na ufundishaji wake kwa ajili ya kuchochea maendeleo endelevu. Mkutano huo umewakutanisha wataalamu kutoka zaidi ya nchi 30, zikiwemo Tanzania, Japan, Sweden na Norway, kwa lengo la kubadilishana uzoefu, maarifa na matokeo ya tafiti pamoja na kujadili namna ya kuendeleza matumizi ya hisabati katika kutatua changamoto za maendeleo. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. William Anangisye, amesema mkutano huo ni fursa muhimu ya kuimarisha ufundishaji wa hisabati kwa wana…