GEHESE YAGEUZA TAKA ZA MASOKONI KUWA FURSA ZA KIUCHUMI
GEHESE YAGEUZA TAKA ZA MASOKONI KUWA FURSA ZA KIUCHUMI
*** Taka zinazozalishwa katika masoko zimeelezwa kuwa zinaweza kubadilishwa kuwa bidhaa zenye thamani na kuwa chanzo cha kipato. Mwanzilishi na Mwenyekiti wa GEHESE, Liliani Lihundi, akizungumza wakati wa warsha ya uhamasishaji na kujenga uwezo kuhusu “Market Waste to Wealth” iliyofanyika Mbezi, Dar es Salaam, amesema usimamizi mzuri wa taka unaweza kusaidia kulinda mazingira na kuongeza fursa za kiuchumi. Lihundi amesema taka za masokoni zinaweza kuchakatwa na kuzalisha mboji, chakula cha mifugo pamoja na bidhaa nyingine. Amesema matumizi ya teknolojia mpya, ikiwemo Black Soldier Fly Larvae (BSFL), yanaweza kuongeza thamani ya taka za kikaboni. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mbezi, Pius Ragiro Nyantori, amesema elimu ya utenganishaji taka inapaswa kupewa kipaumbele katika masoko na jamii. Nyantori amesema Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuanzishwa kwa vituo vya uchakataji taka katika masoko ya kata hiyo. Amesema vituo hivyo vinaweza kuwa kichocheo cha ajira na biashara kwa vi…