FURAHA ILOBASHI! MBUNGE AZZA AAHIDI MIFUKO 150 YA SARUJI KUKAMILISHA NYUMBA YA WALIMU

FURAHA ILOBASHI! MBUNGE AZZA AAHIDI MIFUKO 150 YA SARUJI KUKAMILISHA NYUMBA YA WALIMU
Na Marco Maduhu, SHINYANGA Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu, akiwa ameambatana na wataalamu mbalimbali wa Serikali. TAZAMA VIDEO πŸ‘‡πŸ‘‡ Leo Agosti 5, 2026, Mbunge Azza amefanya ziara katika Kijiji cha Ilobashi, Kata ya Masengwa na Ng'wanhalanga, wilayani Shinyanga. Akizungumza wakati wa kujibu kero mbalimbali za wananchi, likiwamo ombi la kusaidia ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Ilobashi kwa kutoa mifuko ya saruji, Mbunge Azza ameahidi kutoa mifuko 150 ya saruji. "Mimi kama Mbunge ninaahidi kutoa mifuko 150 ya saruji ili kuunga mkono ujenzi wa nyumba hiyo ya walimu katika Shule ya Msingi Ilobashi. Afisa Elimu, nitakapoleta mifuko hiyo ya saruji kwa ajili ya kumalizia sehemu ya juu ya jengo, na halmashauri nayo iangalie namna ya kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo," amesema Azza. Aidha, akijibu kero ya ukosefu wa maji, ameiomba Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini…