ELIMU YA AFYA KUHUSU “ZIJUE NAMBA ZAKO”, MTINDO WA MAISHA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YATOLEWA MANYARA TANZANITE MARATHON
ELIMU YA AFYA KUHUSU “ZIJUE NAMBA ZAKO”, MTINDO WA MAISHA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YATOLEWA MANYARA TANZANITE MARATHON Wizara ya Afya kupitia Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, imetoa elimu ya afya kuhusu mtindo bora wa maisha na Magonjwa Yasiyoambukiza (MYA), pamoja na kutoa huduma za uchunguzi wa afya bila malipo katika viwanja vya mpira vya Kwaraa, Manyara, wakati wa Manyara Tanzanite Marathon. Elimu hiyo imejikita katika kampeni ya “Zijue Namba Zako”, ikiwahamasisha wananchi kufahamu hali ya afya zao kwa kufanya vipimo mbalimbali, ikiwemo uwiano wa urefu na uzito, pamoja na kujenga utamaduni wa kuchunguza afya mara kwa mara ili kubaini changamoto mapema. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Mhe. George Bajuta, amepongeza huduma na elimu hiyo, akisema imekuwa fursa muhimu kwa wananchi kupata elimu na kuchunguza afya zao bila malipo. «“Nashukuru sana Wizara ya Afya kupitia Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwa kuja na programu hii bure katika Manyara Tanzanite Marathon.…