DKT. MWIGULU: BIDHAA ZA TANZANIA ZIWE NA UBORA WA KUSHINDANA KILA SIKU
DKT. MWIGULU: BIDHAA ZA TANZANIA ZIWE NA UBORA WA KUSHINDANA KILA SIKU Na. Meleka Kulwa – Fullshangwe Blog, Dodoma WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa wazalishaji nchini wanapaswa kuboresha ubora wa bidhaa zao ili ziweze kushindana katika soko la kimataifa kila siku, badala ya kuonekana bora wakati wa maonesho pekee. Amesema kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini zinapaswa kufikia viwango vya kimataifa ili kuongeza ushindani, kuvutia wanunuzi na kupanua masoko ya ndani na nje ya nchi, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Ameyasema hayo Agosti 1, 2026, wakati akifungua rasmi Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. John S. Malecela, Nzuguni jijini Dodoma. Aidha, amebainisha kuwa changamoto kubwa katika biashara siyo upatikanaji wa masoko pekee, bali ni ubora wa bidhaa zinazozalishwa, akisisitiza kuwa bidhaa za Tanzania zinapaswa kuwa na kiwango kinachoweza kumshawishi mnunuzi wakati wote. Pia ameongeza kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika uzalishaji wa cha…