DKT. MUNISI: VIONGOZI WA DINI HUBIRINI MAADILI MEMA, DUMISHENI AMANI NCHINI

DKT. MUNISI: VIONGOZI WA DINI HUBIRINI MAADILI MEMA, DUMISHENI AMANI NCHINI
​Na. OWM (KAM) Mwanga ​Serikali imezitaka taasisi na viongozi wa dini nchini kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri maadili mema, mshikamano na uvumilivu ili kujenga jamii yenye amani, utulivu na uchaji wa Mungu. ​Wito huo umetolewa leo, Agosti 30, 2026, na Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Dkt. Evaline Munisi, alipokuwa akizungumza kwenye ibada ya kumwingiza kazini Katibu Mkuu na Mtunza Hazina wa Dayosisi ya Mwanga, iliyoenda sambamba na ubarikio wa wachungaji na uingizaji kazini wa Mwinjilisti. ​Dkt. Munisi ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za dini katika malezi, kuimarisha maadili ya Taifa, pamoja na kutoa huduma za kijamii kama elimu na afya. ​“Taasisi za dini ni wadau muhimu wa maendeleo. Zimekuwa zikifanya kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi kuwa wazalendo, kulinda amani na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii,” amesema Naibu Waziri huyo. ​A…