DC SIMANJIRO AONGOZA KUPASHA MANYARA TANZANITE MARATHON

Na Mwandishi wetu, Mirerani  MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mwalimu Fakii Raphael Lulandala ameongoza mamia ya wakazi wa eneo hilo kwenye mazoezi ya mbio fupi za kujiandaa na Manyara Tanzanite Marathon zinazotarajiwa kufanyika mjini Babati Agosti 22, 2026. Mwalimu Lulandala akizungumza na wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, watumishi wa Halmashauri, wakuu wa vitengo, idara na mashirika amewashukuru kwa kujitokeza kushiriki mbio hizo. “Lengo la mbio fupi za leo ni kujiandaa na kuhamasisha kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kwenye Manyara Tanzanite Marathon itakayofanyika mjini Babati,” amesema Mwalimu Lulandala. Amewaasa watu wa Wilaya hiyo ambao hawajajiandikisha wafanye hivyo kupitia mbio za kilomita tano, 10, 21, na 42 pamoja na kilomita mbili za vijana na watoto. Amesema lengo la mbio hizo ni kuchangia fedha za ujenzi wa wodi na kununua vifaa tiba vya watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda wao wa miezi tisa. Amesema awali wodi hiyo itajengwa kwenye wilaya ya Hanang’ na vi…