CWT YAASWA KUJIKITA KATIKA MAJADILIANO BADALA YA MIGONGANO

CWT YAASWA KUJIKITA KATIKA MAJADILIANO BADALA YA MIGONGANO
Serikali imevitaka vyama vya wafanyakazi nchini, ikiwemo Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kutumia meza ya majadiliano (Social Dialogue) kutatua kero za wafanyakazi badala ya  migongano isiyo na tija inayodhoofisha mshikamano na kushusha morali ya kazi. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Mahusiano Mheshimiwa Dr. Evaline Munisi wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku mbili kwa watumishi wa Makao Makuu na Makatibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa Mikoa na Wilaya kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi hiyo Deus Sangu leo Agosti 13, 2026 mjini Morogoro. Amesema kuwa Vyama vya Wafanyakazi havikuundwa kwa ajili ya kusigana na Waajiri, bali viliundwa kama jukwaa la kisheria la kukaa meza moja na waajiri ili kujadiliana kwa hoja, ushahidi na kuheshimiana. "Vyama vya wafanyakazi havikuundwa kwa ajili ya kusigana na waajiri, bali viliundwa kama jukwaa la kisheria la kukaa meza moja ili kupata suluhu ya pamoja. Katika miaka ya hivi karibuni tumeona kuibuka kwa…