Breaking : MAKAMU WA RAIS TANZANIA DKT. EMMANUEL NCHIMBI ATANGAZA KUJIUZULU

Breaking : MAKAMU WA RAIS TANZANIA DKT. EMMANUEL NCHIMBI ATANGAZA KUJIUZULU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kuanzia Septemba 4, 2026, huku akieleza pia kuwa ameamua kustaafu siasa na utumishi wa umma. Dkt. Nchimbi ametoa taarifa hiyo leo Jumanne, Agosti 25, 2026, akisema amemwandikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha kuhusu uamuzi wake. Katika taarifa yake, Dkt. Nchimbi amesema uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amesema uamuzi huo unatekeleza ahadi aliyompa Rais Samia Agosti 27, 2025, kwamba angemsaidia Rais na nchi kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, huku akiahidi kuachia nafasi hiyo endapo Rais angeona kuna haja ya kuwa na Makamu mwingine wa Rais. “Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu,” amesema Dkt. Nchimbi katika taarifa hiyo. Dkt. Nchimbi pia amemshukuru Rais Samia na Chama Ch…