BODI YA TAFICO YARIDHISHWA KUKAMILIKA KWA BANDARI YA UVUVI KILWA MASOKO

BODI YA TAFICO YARIDHISHWA KUKAMILIKA KWA BANDARI YA UVUVI KILWA MASOKO
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), imefanya ziara ya ukaguzi katika mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko, kwa lengo la kujionea hatua ya utekelezaji wa mradi, kukagua miundombinu na maandalizi yaliyofanyika kuelekea kuanza kwa matumizi ya bandari hiyo, pamoja na kutathmini fursa zitakazotokana na uwekezaji huo katika shughuli za uvuvi na uchumi wa buluu. Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 20 Agosti 2026, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Yunus D. Mgaya, ambapo Bodi hiyo imepata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali ya bandari na kupata maelezo kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya kuanza kwa shughuli zake. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Prof. Mgaya, amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo, akieleza kuwa kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko kutakuwa hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya uvuvi nchini. "Bandari hii ina nafasi kubwa katika kuongeza ufanisi wa shughuli za uvuvi, kuongeza thamani ya mazao ya …