BITEKO: TANZANIA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
BITEKO: TANZANIA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
📌 Asema wajibu wa kila Mtanzania ni kuhakikisha mafanikio yanakuwa endelevu KIZIMKAZI, ZANZIBAR Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanaendelea kuwa endelevu. Dkt. Biteko amesema hayo wakati akishiriki mjadala kuhusu “Uongozi wa Kimkakati wa Tanzania katika Kuharakisha Mabadiliko ya Nishati Endelevu na Jumuishi”, uliofanyika katika Mdahalo wa Nishati Safi ulioandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF), Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Amesema uwepo wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia ni sehemu ya jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuipa msukumo ajenda hiyo katika ngazi mbalimbali za uongozi wake na kuifikisha hadi katika majukwaa ya kimataifa. Dkt. Biteko amesema …