ALBAN KIHULLA ASISITIZA MATUMIZI YA VIPIMO SAHIHI KATIKA BIASHARA YA KAHAWA MBINGA

ALBAN KIHULLA ASISITIZA MATUMIZI YA VIPIMO SAHIHI KATIKA BIASHARA YA KAHAWA MBINGA
Vipimo sahihi kwa kutumia mizani iliyohakikiwa na WMA. Kiwanda cha Twende Shamba Tanzania Ltd. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Alban Kihulla, Kulia ni Meneja (WMA) Mkoa wa Ruvuma (Nyagabona Mkanjabi) na kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Twende Shamba Tanzania Ltd ( Bw. Ngapomba) *** 14 AGOSTI 2026 Na. WMA – MBINGA, RUVUMA Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Alban Kihulla, ametembelea kiwanda cha Twende Shamba Tanzania Ltd kilichopo Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, kinachojihusisha na ununuzi wa kahawa kutoka kwa wakulima wadogo pamoja na uchakataji wa zao hilo tarehe 14 Agosti, 2026. Ziara hiyo imelenga kujionea kwa karibu shughuli za uzalishaji na uchakataji wa kahawa, pamoja na kuhakikisha kuwa vipimo sahihi vinazingatiwa katika kila hatua ya mnyororo wa ukusanyaji wa kahawa. Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kihulla, amesisitiza umuhimu wa matumizi ya vipimo sahihi katika kuhakikisha haki, uwazi na uaminifu katika biashara ya kahawa unazingatiwa, …