WIZARA YA ELIMU YAANZA MAGEUZI MAKUBWA KUJIBU MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA
WIZARA YA ELIMU YAANZA MAGEUZI MAKUBWA KUJIBU MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA Na Dotto Kwilasa,Dodoma WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza utekelezaji wa mkakati mpya unaolenga kuifanya sekta ya elimu izalishe wahitimu wenye ujuzi, ubunifu na uwezo wa kushindana katika soko la ajira la ndani na kimataifa, sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Mkakati huo unajumuisha maboresho ya mitaala, matumizi makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano, ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uwekezaji wa elimu pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya kupanga na kufanya maamuzi. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Caroline Nombo,amesema mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya elimu yanapaswa kuwa chachu ya kuharakisha mageuzi yanayolenga kuandaa rasilimali watu itakayokidhi mahitaji ya uchumi wa kisasa. Akizungumza leo July 13,2026 kwenye Kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Pro…