WIZARA, TAASISI NA UMMA NA BINAFSI NA MASHIRIKA YA KIRAIA YAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA MKUTANO WA COP 12

WIZARA, TAASISI NA UMMA NA BINAFSI NA MASHIRIKA YA KIRAIA YAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA MKUTANO WA COP 12
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Rueben Kwagilwa akizungumza na vyombo vya habari Julai 2,2026 Jijini Tanga kuhusu tamko la Serikali kuhusiana na maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP 12) unaotarajiwa kufanyika Kuanzia Octoba 6 hadi 9 Mwaka huu Serikali imezitaka Wizara, Taasisi za Umma, Sekta Binafsi, Watafiti na Mashirika ya Kiraia kuchangamkia fursa ya Tanzania kuwa mwenyeji wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP 12). Hayo yamesemwa leo Julai 2, 2026 Jijini Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Reuben Kwagilwa wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano huo unaotarajia kufanyika nchini kuanzia tarehe 6-9 Oktoba mwaka huu. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian akionesha kitabu chenye taarifa ya utafiti kuhusu masuala ya mazingira mkoani humo wakati wa mkutano wa Naibu Waziri Ofisi ya Makau a Rais (Muungano na Mazingira )Mhe…