WAZIRI WA ULINZI AIPONGEZA JKT NA JWTZ KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA NCHINI

WAZIRI WA ULINZI AIPONGEZA JKT NA JWTZ KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA NCHINI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, amewapongeza viongozi wa  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa juhudi wanazozifanya za kuimarisha ulinzi na usalama nchini. Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam  Sabasaba, Julai 6, 2026, amesisitiza kuwa vyombo hivyo vya ulinzi vimekuwa vikiendelea kulinda amani ya nchi, jambo linalowezesha wananchi kufanya shughuli za maendeleo na kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050. Aidha amesema shirika  la JKT linafanya kazi za uzalishaji mali pamoja na kuwafundisha vijana, hatua inayosaidia kuwaandaa kujitegemea na kujiajiri. Ameeleza kuwa kupitia maonesho hayo, taasisi hizo zimepata nafasi ya kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye vikosi vyao, ikiwemo kutoa huduma kwa wananchi na mafunzo kwa vijana. Amesema kampuni ya usafi na unyunyuzi dawa ya SUMA JKT ambayo imef…