WAZIRI SHEMDOE AIPONGEZA TARURA KWA KAZI KUBWA YA KUUNGANISHA MAENEO YA VIJIJINI KUPITIA MIUNDOMBINU YA BARABARA
WAZIRI SHEMDOE AIPONGEZA TARURA KWA KAZI KUBWA YA KUUNGANISHA MAENEO YA VIJIJINI KUPITIA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA FARIDA MANGUBE Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Prof. Riziki Silas Shemdoe (Mb), ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi kubwa ya kuunganisha mawasiliano ya barabara kutoka kijiji hadi kijiji na wilaya hadi wilaya, akisema kuwa jukumu hilo ni gumu na linahitaji weledi, uzalendo na utendaji wa hali ya juu. Prof. Shemdoe alitoa pongezi hizo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Isago lenye urefu wa mita 42.6 katika Kata ya Mngeta, Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, mkoani Morogoro, akiwa katika ziara ya kikazi ya tarehe 2 hadi 6 Julai 2026 Mkoani humo. Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya mradi iliyosomwa na Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Ndyamukama, Waziri Shemdoe amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya barabara na madaraja ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi. “TARURA mmefanya kazi kubwa sana ya kuunganisha…