WAZIRI SANGU AKUTANA NA MZEE WA UPAKO NA MTUME MALISA
WAZIRI SANGU AKUTANA NA MZEE WA UPAKO NA MTUME MALISA
-Aeleza umuhimu wa Mahusiano mema katika kuimarisha mshikamano wa Taifa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, leo Julai 4, 2026 Jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mchungaji Antony Thomas Lusekeleo maarufu kama Mzee wa Upako wa Kanisa la Gospel Revival Centre (GRC) pamoja na Mtume Crear Malisa wa King Dom Embassy Church, ambapo viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano wa Serikali na Taasisi za Dini katika kukuza ustawi wa jamii na mshikamano wa kitaifa. Katika mazungumzo hayo, Waziri Sangu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilianzisha Idara maalumu ya Mahusiano chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuimarisha uratibu wa masuala ya kijamii na kitaasisi, ikiwemo mahusiano ya kazi, mahusiano kati ya serikali na wadau wa kijamii, vyama vya siasa na taasisi za dini. Pia, kukuza amani, umoja na mshikamano katika jamii. Waziri Sangu alibainisha kuw…