WAZIRI MAVUNDE AANZA ZIARA RASMI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI MKOANI GEITA

WAZIRI MAVUNDE AANZA ZIARA RASMI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI MKOANI GEITA
▪️ Waziri Mavunde ni Mlezi wa shughuli za kimaendeleo mkoani Geita* *▪️ Akagua mradi wa maji wa Bilioni 40 ambao utanufaisha watu 185,000* *▪️ Akagua mradi wa vijana wa ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua madini* *▪️ Aweka jiwe la msingi ujenzi wa Daraja la Rwantaba* *Chato, Geita** Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameanza ziara rasmi ya kikazi mkoani Geita kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuhamasisha shughuli za kiuchumi na kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayolenga kuboresha maisha ya wananchi. Mhe. Mavunde, ambaye pia ni Mlezi wa shughuli za maendeleo mkoani Geita, anatarajiwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa katika halmashauri na wilaya za mkoa huo, sambamba na kuzungumza na wananchi kuhusu fursa za maendeleo na mchango wa sekta ya madini katika kukuza uchumi wa Taifa. Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Waziri Mavunde amekagua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 40, unaotarajiwa kun…