WAZIRI KIJAJI AIPA KONGOLE TAWA KWA KUVUTIA WAWEKEZAJI

WAZIRI KIJAJI AIPA KONGOLE TAWA KWA KUVUTIA WAWEKEZAJI
Na Beatus Maganja, Morogoro Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa mafanikio yake katika kuvutia wawekezaji jambo lililotajwa kuchangia ongezeko la mapato ya Taasisi hiyo, huku akiielekeza Menejimenti ya mamlaka hiyo kuandaa mikakati ya muda mfupi, ya kati na ya muda mrefu ya kudhibiti migongano baina ya wanyamapori na binadamu. Akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TAWA alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA mkoani Morogoro Julai 7, 2026, Dkt. Kijaji alisema mwaka mpya wa fedha unapaswa kuwa mwanzo wa utekelezaji wenye matokeo makubwa katika kuimarisha uhifadhi wa maliasili na kuongeza kasi ya kudhibiti migongano kati ya binadamu na wanyamapori ili kuhakikisha usalama wa wananchi na wanyamapori kwa pamoja. "Tunapaswa kuwa na mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu itakayowezesha kupunguza migongano kati ya wanyamapori na binadamu. Lengo letu ni kuona wan…